Katika kutekeleza Mkataba wa Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Pangani imeendelea kutekeleza afua mbalimbali za Lishe.
Ambapo moja ya afua muhimu inayotekelezwa ni maadhimisho ya Siku ya afya na Lishe yanayofanyika kila robo kwa kila kijiji.
Katika kutekeleza mkataba huo kijiji cha Mtonga leo tarehe 13 Disemba 2023 kimefanya maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe( SALiKi) ambapo jumla ya wananchi 242( 176Ke na 66Me) wamehudhuria na kupatiwa Elimu ya Lishe na Elimu nyingine jumuishi kutoka sekta ya Kilimo,mifugo na uvuvi.
Aidha, jumla ya watoto 132 wamepimwa hali zao za lishe na hali zao wote ziko vizuri(wote kipimo kimeonyesha alama ya kijani).
Pamoja na hayo huduma zingine zimetolewa ikiwemo kutoa matone ya Vitamini A na kufanya mapishi ya mfano.
#panganimpya
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa