Halmashauri kupitia idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu, wameandaa na kutoa Mafunzo elekezi ya utumishi wa umma leo Novemba 1,2023, kwa Watumishi wapya wa Kada mbalimbali walioajiriwa mwaka wa fedha 2022/2023 hadi 2023/2024, katika ukumbi wa zamani wa Halmashauri na kuhudhuliwa na Kamati ya Fedha,Mipango na Uongozi chini ya Mwenyekiti mhe Akida Bahorera.
Akiongoza mafunzo hayo Mkuu wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu Bi Veronica Marwa,ametoa rai kwa Watumishi wapya kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia misingi,sheria na miongozo ya Serikali kwa maslahi mapana ya kulitumikia Taifa kwa ujumla.
Aidha kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani bw. Isaya M Mbenje, ameendelea kuishukuru Serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais Mhe. Dkta. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kutoa fursa za ajira kwa watumishi wapya kwa lengo la kuwahudumia wananchi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani mhe Akida Bahorera, amewapongeza watumishi wote wapya waliofanikiwa kupata ajira na kupangiwa katika Wilaya ya Pangani na kuendelea kuwahimiza kutumika katika nafasi zao kwa uadilifu na kutatua changamoto zote zilizopo katika jamii.
Mafunzo haya elekezi yenye lengo la kuwajengea uwezo na utendaji bora kwa ajira mpya katika utumishi wa umma, yanatarajiwa kuhitimishwa Novemba 2,2023.
#panganimpya
#kaziiendelee
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa