Batilda Azipongeza Halmashauri Zote za Mkoa wa Tanga kwa Kupata Hati Safi
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Batilda Burian, amezipongeza Halmashauri zote za mkoa huo kwa kupata hati safi katika mwaka wa fedha 2023/2024.
Mhe. Batilda alitoa pongezi hizo leo, Juni 16, 2025, wakati wa kikao maalum cha Baraza la Madiwani kilichoitishwa kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ukumbi wa Halmashauri ya zamani Wilayani Pangani.
Amesema matokeo hayo chanya ni ishara ya uwajibikaji, usimamizi thabiti wa rasilimali za umma, na mshikamano kati ya viongozi, watendaji na wananchi katika mkoa wa Tanga. Aidha, amezitaka halmashauri kuendelea kuimarisha mifumo ya ndani ya udhibiti na kuhakikisha matumizi ya fedha za umma yanazingatia sheria, taratibu na kanuni.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa