Halmashauri ya wilaya ya Pangani yashika nafasi ya kwanza kimkoa (TANGA)Matokea ya kidato cha nne yaliyotangazwa mnamo tarehe 24/01/2019
Kwa mwaka wa fedha 2017/2018 Tumetoka kuwa Wilaya ya 164 (2017) na sasa Wilaya ya 50 (2018) Halmashauri zote nchini.akiongea mara baada ya kutangazwa matokeao hayo mkuu wa wilaya ya Pangani alisema “Pangani tumeamua kuweka kipaumbele chetu cha kwanza kwenye elimu na tumesimamia kwa vitendo
Tulifanya ziara kwa kushirikiana na viongozi wa chama na serikali ndani ya vijiji vyote 33 na tukatembelea shule zote za serikali na Binafsi kuhamasisha chachu ya ufaulu.
Ushirikiano na kufanya kazi kwa bidii kwa viongozi wilaya ya Pangani kuanzia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya chini ya DC,DAS,Afisa Tawala na Maafisa Tarafa pia Halmashauri chini ya Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Halmashauri na zaidi Mbunge.
Alielezea mambo saba yaliyochangia Halmshauri kupata matokea hayo ambayo ni pamoja na
1.Kuhakikisha kila shule wanafanya mitihani ya majaribio kila wiki, kwa kata kila mwezi, kwa wilaya kila baada ya miezi mitatu na mkoa kila baada ya miezi sita. Na mitihani hii ishindanishe government na private schools ili tujue status ya shule zetu za serikali ikoje.
2. Kuhakikisha kila shule kuna upatikanaji wa chakula. Wanafunzi wanaokula vizuri na umakini wao darasani huongezeka.
3. Kuboresha miundombinu ya shule kwa kuhakikisha kila kaya wanachangia matofali 5 ambayo ni sawa na shilingi 7,500/= kwa kaya. Fedha hizi zikipatikana zisaidie kupunguza changamoto ya uhaba wa madarasa na matundu ya vyoo mashuleni.
4. Madarasa ya mitihani wanafunzi wote wakae kambi ili wapate mda wa kutosha wa kujisomea na kujiaandaa na mitihani.
5. Walimu na wanafunzi watakao fanya vizuri wapatiwe motisha ili waendelee kufanya vizuri zaidi.
6. Kuhakikisha tunapunguza au kuondoa mimba na ndoa za utotoni kwa kufuata sheria. Iundwe kamati ya wilaya ya kufuatilia maadili ya wanafunzi na walimu;
7. Kuwe na vikao vya mara kwa mara kuwahimiza wazazi juu ya umuhimu wa elimu na kufuatilia mara kwa mara progress za watoto wao.
Tumedhamiria kusimamia kipaumbele chetu cha Elimu na tunatarajia kufikia malengo ya kuiinua wilaya hii ambayo ukombozi wake na urithi ni Elimu
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa