Hatimaye, ndoto ya maji safi na salama kwa wakazi wa Kijiji cha Mkwaja, Wilayani Pangani inatimia
Kupitia upanuzi wa mradi wa maji kutoka Mikocheni, jumla ya wananchi 2,081 watanufaika moja kwa moja kupitia Vituo 13 vya kuchotea maji (DPs) vilivyokamilika pamoja na Maunganisho ya maji majumbani yanayoendelea.
Lengo kuu la mradi huu ni kuondoa adha ya ukosefu wa maji safi na kuimarisha afya, elimu na maendeleo ya kiuchumi kwa jamii ya Mkwaja.
Ofisi ya RUWASA Wilaya ya Pangani kwa niaba ya wananchi wa kijiji cha Mkwaja inatoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa fedha za ujenzi wa mradi huu ambao utawapunguzia wanajamii wa kijiji cha Mkwaja adha ya kutumia muda mrefu wa kutafuta maji badala ya kutumia muda huo kwenye shughuli za kiuchumi.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa