Ujenzi wa Jengo la Mama, Baba na Mtoto zahanati ya kimang'a wilayani Pangani umekamilika.Akipokea taarifa hio 17 Julai 2023 mkuu wa wilaya ya Pangani Mh. Zainab Abdallah akiwa na timu yake ya ulinzi na usalama wilaya pamoja na wakuu wa idara na vitengo wa halmashauri ya wilaya ya Pangani wakati wa ziara ya twende na samia kijiji kwa kijiji, amesema kuwa "tunaishukuru sana sana serikali ya awamu ya sita kwa kuwajali wananchi wa kimang'a kwa kuwezesha kupata fedha kwaajili ya ujenzi wa jengo hili zuri na la kisasa la mama,baba na mtoto,ni matumaini yangu kuwa jengo hili litatoa huduma bora kwa jamii yetu".Aidha mkuu wa wilaya ametoa pongezi kwa Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha milioni 50 pamoja na wanakijiji wa Kimang'a kwa kujitoa na kushiriki mchakato mzima wa ujenzi wa jengo hilo la mama, baba na mtoto
#panganimpya
#kaziiendelee
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa