Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani ndg Juma Mbwela amewashukuru Wataalam wote kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi na Wizara ya Afya kwa kushiriki moja kwa moja katika Kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi kuhusu Kampeni ya Kitaifa ya Chanjo ya Surua na Rubella, na amewahakikishia kuwa atakuwa mstari wa mbele kuhakikisha zoezi hilo la Chanjo linafanikiwa kwa Asilimia zote na linamgusa kila Mtoto na kwa wakati.
Hayo ameyasema leo tarehe 14 Februari, 2024 katika ukumbi wa Halmashauri ya Zamani.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii ambae pia ni Diwani wa Kata ya Pangani Mashariki mhe Akida Boramimi ametoa wito kwa Wananchi kushiriki kikamilifu katika kufanikisha zoezi la utoaji chanjo kwa manufaa ya Wilaya ya Pangani.
Aidha timu ya Wataalam mbalimbali kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi na Wizara ya Afya wamefafanua baadhi ya faida za Chanjo ya Surua na Rubbela, ikiwemo usalama wa Chanjo hizo pamoja na faida zake kwa Watoto.
Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Pangani ndg Ester Gama amewataka waratibu wa zoezi hilo la Chanjo kuhakikisha wanafuata miongozo ya Wizara na kuwafikia watoto wote wanaostahiri kupatiwa chanjo hiyo muhimu.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa