Kamati ya Afya ya Msingi ya Halmashauri ya Wilaya ya Pangani imefanya kikao kujadili zoezi la uhamishaji wa Makaburi yatakayo athiriwa na ujenzi wa barabara ya kutoka Pangani hadi Makurunge, hii ni baada ya kupokea barua kutoka kwa Meneja wa Wakala wa barabara.
Kikao hicho kimefanyika leo Januari 3, 2023 katika ukumbi wa Zamani wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani.
Akifungua kikao hicho kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Katibu Tawala Wilaya ya Pangani ndg Ester Gama amesema kuwa jumla ya Vijiji 8,vilivyopo Pangani vimeathiriwa na Mradi huo na miongoni mwa Vijiji hivyo ni pamoja na kijiji cha Pangani Magharibi , Bweni ,Mzambarauni,Mwera,Mikinguni,Tungamaa, Makorora pamoja na Mikocheni vyenye jumla ya Makaburi 348.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo ndg Timothy Mgaya Afisa Afya amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani imepokea jumla ya Shilingi milioni 122,437,500 kutoka kwa Wakala wa barabara(TANROAD) kwaajili ya Uhamishaji wa Makaburi,ambapo kiasi cha milioni 91,477,500 ni uhamishaji wa makaburi 258 kwa Lot 2 na milioni 30,960,00 ni uhamishaji wa Makaburi 90 kwa Lot 3.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii mhe Akida Boramimi amesema kuwa zoezi hili linagusa moja kwa moja ushiriki wa Wananchi katika eneo husika na ametoa wito kwa kila anaestahiki aweze kupata stahiki yake.
Aidha bwa. Bora Mimi amewataka Viongozi katika Serikali za Vijiji kufanya Mikutano ya Hadhara kutaarifu umma uwepo wa zoezi hili.
Zoezi hilo litahusisha shughuli muhimu zikiwemo, Ununuzi wa Vitendea Kazi, pamoja na Zoezi la Ufukuaji na Uzikaji upya wa Makaburi yatakayo athiriwa na Mradi.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa