Aprili 18,2024, Kamati ya Fedha, Mipango na Uongozi ya Halmashauri ya Wilaya ya Pangani ikiongozwa na Mhe Akida Bahorera Mwenyekiti wa Halmashauri,imekagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kamati hiyo imekagua ujenzi wa Madarasa 4 na Matundu 7 ya Vyoo kwa kidato cha 5 na 6 Shule ya Sekondari Bushiri, Ukarabati wa madarasa 2 Shule ya Msingi Boza, Ujenzi wa Jengo la Makao makuu ya Halmashauri pamoja na ukarabati wa hospitali ya Wilaya.
Akiwasilisha taarifa za miradi hiyo Afisa Mipango Bw. Saimon Vedastus amesema kuwa anaishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais wake mhe dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha miundombinu mbalimbali katika Wilaya ya Pangani.
" Tumeendelea kupokea fedha kwaajili ya miradi ya maendeleo, hivyo tunaendelea kuisimamia kwa ukaribu ili iweze kutoa huduma stahiki katika jamii zetu".
Aidha Kamati ya fedha imetoa ushauri na mapendekezo kwenye mapungufu yaliyo bainika katika miradi hiyo nakuazimia kurudi kukagua na kuangalia namna ya maboresho hayo pamoja na utekelezaji wake kufikia Aprili 15,2024.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa