Pangani_Tanga
Wajumbe wa Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Akida Bahorera Oktoba 16,2023 wametembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo katika kipindi cha robo ya Kwanza 2023/2024.
Hata hivyo Kwa upande wake Mhe. Akida Bahorera amesisitiza wananchi kutunza miundombinu inayotekelezwa na Serikali katika maeneo yao.
Kwa upande wake mjumbe wa kamati hii Mhe Akida Boramimi amewapongeza wasimamizi wa miradi na kuwaomba kuongeza bidii katika kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati na ubora.
Vilevile Mradi wa Ujenzi wa Vyumba 2 Madarasa na Matundu 3 ya Vyoo Shule ya Msingi Pangani, wenye thamani ya shilingi Milioni 56.3 fedha kutoka Serikali Kuu ambapo Mradi huo wa madarasa umekamilika na unaendelea kutumika.
Miradi iliopata nafasi ya kutembelewa na kukaguliwa na kamati hii ni Pamoja na ujenzi wa madarasa 7 na mabweni 2 shule ya Sekondari Mwera ambapo madarasa yote yamekamilika ,mabweni yapo katika hatua za ukamilishaji kazi inayoendelea ni uwekaji wa sakafu na mifumo ya maji.
#panganimpya
#elimubora
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa