Pangani_Tanga
Wajumbe wa Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Akida Bahorera leo Januari 18,2024 wametembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo Wilayani Pangani.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa Wash katika Zahanati ya Kigurusimba ndg Revocatus amesema kuwa Ujenzi ulianza tarehe 26 Novemba 2023 na unatarajiwa kumalizika tarehe 31 Januari 2024.
Ameongeza kuwa hadi sasa mradi upo katika asilimia 85 ambapo ujenzi wa kichomea taka, shimo la kondo la nyuma na shimo la majivu vimekamilika.
Akiongea mala baada ya kukagua miradi hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri mhe Akida Bahorera amewataka wasimamizi wa miradi hiyo kuongeza umakini katika kusimamia ili miradi hiyo iweze kukamilika kwa wakati na kutatua kero za Wananchi.
Kwa upande wa mradi wa ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari Masaika, katibu wa ujenzi ndg Mackrella Mruthu amebainisha kuwa moja ya mafanikio ya mradi huu ni pamoja na Shule kusajiliwa na kupewa namba ya Usajili na tayari jumla ya wanaafunzi 79 wa kidato cha kwanza wamejiunga na wanaendelea na masomo yao
Vilevile miundombinu yote kusudiwa ikiwepo ujenzi wa tenki la maji,Vyoo na madarasa imekamilika kwa asilimia 98.
Miongoni mwa miradi iliyopata nafasi ya kukaguliwa ni mradi wa Ujenzi wa Vyoo Shule ya msingi Kimang'a, Shule ya Sekondari Masaika, Zahanati ya Bushiri, ujenzi wa Bweni la Wanafunzi wenye mahitaji maalumu Shule ya Msingi Funguni, pamoja na Shule ya Msingi Masaika.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa