Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe Akida Bahorera imeketi leo Agosti 30, 2024 kujadili Hesabu za Mwisho za Mwaka 2023/2024 za Halmashauri.
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa makao makuu ya Halmashauri, (Mkoma).
Akiwasilisha taarifa za Hesabu hizo Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Uhasibu ndg Salim Lugelo amesema kuwa Taarifa zinazowasilishwa leo ni pamoja na taarifa ya Mizania, mapato na matumizi, mtiririko wa fedha, mabadiliko ya rasilimali halisi na tini ya taarifa za fedha.
Ndg Salim Lugelo amefafanua kuwa Halmashauri imeweza kusimamia vizuri ukusanyaji wa Mapato ya ndani na imekusanya shilingi Billioni 1.8 ya lengo la Shilingi Bilioni 1.9 sawa na asilimia 94. Kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Ameeleza kuwa Halmashauri imeendelea kupokea fedha kutoka Serikali kuu ikijumuisha mishahara ya watumishi,Tasaf,elimu bila malipo,SEQUIP, BOOST, Ununuz wa vifaa tiba na miradi mingine ya maendeleo.
Aidha kamati ya FUM imesisitiza Menejimenti kuendelea kukusanya mapato kwa bidii kwa mwaka wa fedha 2024/2025 na kufikia asilimia 100, na kuhakikisha fedha za Serikali zinatumika ipasavyo katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa