KAMATI YA HUDUMA ZA JAMII KIJIJI CHA MADANGA , YAPITISHA MAJINA YA WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII.
Shirika la AMREF Health Africa kwa kushirikiana na Wizara ya Afya pamoja na Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wanasimamia zoezi la kuwachagua na kuwapigia kura Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kupitia mradi wa Afya Himilivu.
Pichani ni wajumbe wa kamati ya huduma za jamii ya kijiji cha Madanga wakipitia na kuchambua orodha ya waombaji waliokizi vigezo vya kuchaguliwa kuwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii.
Zoezi la upigaji kura litafanyika leo Septemba 11,2024 katika kitongoji cha Madanga na watakaochaguliwa watapata fursa ya kupatiwa elimu kabla ya kuwatumikia wananchi katika nafasi ya mhudumu wa afya ngazi ya jamii.
Kwa upande wao wataalam kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Wizara ya Afya na Amref kwa pamoja wamefurahishwa na taratibu zote zilizotumika kuhakikisha uchaguzi unafanyaka kwa haki na usawa, ili kupata wahudumu wenye weledi kuwatumikia wananchi.
Ikumbukwe kuwa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii ndio Mstari wa mbele katika Sekta ya Afya wanaoweza kuibua wagonjwa na kutoa taarifa zote kuhusu masuala ya Magonjwa ikiwemo yasiyoambukiza na yakuambukiza na kuisadia jamii kwa haraka.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa