Kamati ya Lishe Wilaya ya Pangani yafanya Kikao cha Utekelezaji wa Afua za Lishe.
Kikao hicho kimefanyika leo Mei 7, 2024 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri chenye lengo la kupokea na kujadili utekelezaji wa Afua za Lishe kwa kwa kipindi cha robo ya Tatu (Januari - Machi 2024.)
Akifungua kikao hicho kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji ndg Ramadhani Zuberi, amewataka wajumbe wa kikao kufahamu kuwa kikao hicho ni muhimu katika uboreshaji wa lishe katika jamii na kuwasihi kusimamia afua za lishe kwenye maeneo yao kwa kuzingatia vigezo vya Kitaifa ili kuwa na Jamii yenye afya bora.
Awali akieleza mafanikio katika utekelezaji wa viashiria vya lishe vinavyopimwa na Mkataba kwa Ngazi ya Wilaya, Afisa Lishe Wilaya ndg Daudi Mwakabanje amesema viashiria vyote 14 vinavyopimwa katika utoaji wa huduma za lishe katika Wilaya ya Pangani vimetekelezwa vizuri(Viashiria vyote rangi ya Kijani) katika kipindi cha robo ya Tatu kuanzia mwezi Januari hadi Machi 2024.
Sambamba na hilo, amewasisitiza Wakuu wa Shule za Sekondari na Msingi kuendelea kuhakikisha wanasimamia utoaji wa huduma ya chakula mashuleni ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo suala la lishe katika uongozi wa Awamu ya Sita ni kipaumbele.
Taarifa za Utekelezaji wa afua za lishe kutoka sekta mtambuka zilizowasilishwa ni pamoja na idara ya huduma za afya ,ustawi wa Jamii na Lishe,idara ya Elimu Awali na Msingi,idara ya Elimu Sekondari,idara ya Maendeleo ya Jamii, idara ya Mipango na Uratibu pamoja na idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa