Kamati ya Lishe yafanya Kikao cha kujadili taarifa za utekelezaji wa Afua za Afya na Lishe kwa Kipindi cha Robo ya PILI OKTOBA- DISEMBA, 2023/2024.
Kamati ya Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Pangani leo Februari 15, 2024 imefanya Kikao cha kawaida katika Ukumbi wa Halmashauri, Kujadili na Kupokea taarifa za utekelezaji wa Afua za Afya na Lishe kwa kipindi cha Robo ya Pili kuanzia Oktoba hadi Disemba 2023/2024.
Akifungua kikao hicho kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Bw. Simeon Vedustus amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani inatekeleza Afua za Lishe kwa vitendo kwani Serikali ya Tanzania imeendelea kulipa umuhimu suala la Lishe bora.
"Taifa likiwa na watu wenye Afya basi shughuli zinafanyika kwa ubora na usahihi, hivyo ni jukumu letu kulisimamia vizuri suala hili kwa manufaa ya vizazi vyetu".
Kwa upande wake Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani ndg Daud Mwakabanje amesema kuwa shughuli mbalimbali za utekelezaji wa Afua za Lishe zimefanyika na zimeleta faida kubwa, utoaji wa Elimu ya Chakula na Afya zimetolewa Shuleni, pamoja na upimaji wa uwiano wa uzito na urefu, kwa kipindi cha robo hii ya Pili.
Aidha, katika kikao hicho wajumbe wameahidi kuongeza jitihada zaidi kuhamasisha na kutoa Elimu kwa Wananchi juu ya masuala ya Lishe ili kuboresha Afya.
Divisheni mbalimbali ziliwasiliisha taarifa za utekelezaji wa Afua za Afya na Lishe kwa kipindi cha robo ya Pili, ikiwemo Divisheni ya Huduma za Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe , Idara ya Mipango na Uratibu, Elimu Awali na Msingi, Elimu Sekondari, Idara ya Maendeleo ya Jamii, pamoja na Idara ya Fedha na Mipango.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa