Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga chini ya Mwenyekiti wake mhe Rajabu Abdullarhman leo Septemba 24,2024 imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo,Wilayani Pangani
aidha kamati imekagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa matundu 03 ya Vyoo vya wagonjwa, matundu 02 ya vyoo vya watumishi, kichomea taka,ujenzi wa kinawia mikono pamoja na ujenzi wa mnara wa Tanki la maji, Zahanati ya Bushiri.
Akiwasilisha taarifa ya mradi huo Mtendaji wa Kata ya Bushiri Bi Athumini Juma amesema jumla ya shilingi milioni 53, fedha kutoka Serikali kuu zilipokelewa kwaajili ya ujenzi wa mradi huu hadi sasa mradi upo asilimia 90 za ukamilishaji.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa mkoa wa Tanga mhe Rajabu Abdullarhama n amesema kuwa miradi hii inalenga kuwasaidia wananchi wote wa Pangani,
" Mhe Rais anatuletea fursa mbalimbali tujitokeze kuzichukua fursa zote, kwa maendeleo ya Wilaya yetu". nawapongeza kwa kufanya kazi hii kwa uaminifu mmeonyesha uungwana kwa kusimamia fedha alizoleta mhe Rais". Alisema.
Aidha ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Pangani kwa kuwa wawazi na kutoa fursa kwa wananchi kushiriki kwenye mirahi hiyo.
Zahanati ya Bushiri inatoa huduma kwa wananchi zaidi ya elfu 4700.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa