Kamati ya Siasa Wilaya ya Pangani, chini ya uongozi wa Mwenyekiti wake, Mhe. Abdallah Mahmoud, imefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika wilaya hiyo.
Ziara hiyo ilifanyika leo, tarehe 22 Januari 2025, na ilihusisha miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa mabweni 02, madarasa 05, matundu 08 ya choo katika Shule ya Sekondari Mwera, ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mikinguni, ukamilishaji wa vyumba 04 vya madarasa na maabara Shule ya Sekondari Jumaa Aweso, mradi wa usafi katika Zahanati ya Kipumbwi kupitia (SRWSSP), na ukarabati wa miundombinu ya maji Kijiji cha Sange.
Katika ziara hiyo, Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya, Mhe. Abdi Swala, alitoa pongezi kwa Mkuu wa Wilaya, Mhe. Gift Isaya Msuya, mhe Mbunge wa jimbo la Pangani mhe Jumaa Aweso, Mwenyekiti wa CCm Mkoa wa Tanga na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyo, akisisitiza kuwa ni muhimu miradi hiyo iendelee kusimamiwa vizuri ili kutoa huduma bora kwa wananchi kwa wakati.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Mhe. Abdallah Mahmoud, pia alisisitiza umuhimu wa usimamizi bora wa miradi na kutoa pongezi kwa wakandarasi kwa kazi nzuri wanayoifanya.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa