"Kikao hiki kinatoa fursa ya kujadili maendeleo ya Wilaya hivyo ni muhimu makundi yote muhimu kushiriki ili kila mmoja apate fursa ya kuona maendeleo,ni Muhimu kuwashirikisha wadau wote wa maendeleo".
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Pangani Mh. Zainab Abdallah ambae ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) kwenye kikao cha tarehe 12/09/2023 katika Ukumbi wa Zamani wa Halmashauri, kilichohudhuriwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Katibu Tawala, Wakuu wa Idara na Vitengo,Viongozi mbalimbali wa Dini, Viongozi wa Vyama Vya Siasa na Wataalamu mbalimbali wa Halmashauri ya Pangani, Pamoja na Wajumbe mbalimbali.
Lengo la kikao hicho ilikua ni kujadili taarifa mbalimbali zautendaji kazi wa halmashauri na taasisi zote zilizopo ndani ya wilaya ya Pangani.
Katika Kikao hiki,taarifa ya utekelezaji wa Bajeti iliwasilishwa na Idara ya Mipango na Uratibu na Bwan Emmanuel Mbonde Afisa Uchumi, inayoonesha malengo na mafanikio ya Mwaka wa Fedha 2023/2024.
Wajumbe wametoa ushauri na maoni mbalimbali ili kuboresha maendeleo ya Wilaya ya Pangani.
#panganimpya
#kaziiendelee
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa