Leo, tarehe 3 Septemba 2025, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Pangani, SSP Sophia, akiwa pamoja na waratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto wilayani, wamefanya muendelezo wa utoaji wa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Funguni.
Hii ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya “TUWAAMBIE KABLA HAWAJAHARIBIWA"awamu ya pili uliyo zinduliwa na mkuu wa jeshi la polisi Tanzania tarehe 04/08/2025 huko jikoni Dar es salaam,inayolenga kuongeza uelewa kwa watoto na vijana juu ya haki zao, namna ya kujikinga na ukatili wa kijinsia, na jinsi ya kuripoti matukio yanayoweza kuwahusisha.
Mkuu wa Polisi, SSP Sophia, amesisitiza kuwa elimu kama hii ni muhimu katika kulinda afya na ustawi wa watoto na vijana, na aliwataka wadau wote kushirikiana katika kuanda mazingira salama kwa watoto.
Wanafunzi walipata nafasi ya kuuliza maswali na kushiriki mijadala kuhusu changamoto wanazokutana nazo, huku wakipatiwa mwongozo wa kujiweka salama dhidi ya ukatili wa kijinsia.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa