Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Rashid Mchatta ( mwenye kofia), leo tarehe 2 Julai 2025, ametembelea na kukagua maendeleo ya maandalizi ya vipando na mabanda ya maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki, banda la Halmashauri ya Wilaya ya Pangani.
Mchatta amejionea hatua mbalimbali zilizofikiwa katika maandalizi ya mashamba ya mfano, bustani, na mabanda ya maonyesho ya taasisi za serikali, binafsi na vikundi vya wakulima. Amewapongeza wataalamu wa kilimo na wadau wote kwa maandalizi mazuri yanayoendelea kufanyika.
Amesisitiza umuhimu wa ubunifu na uwasilishaji bora wa teknolojia zitakazowezesha wakulima kupata maarifa ya kisasa yatakayoboresha uzalishaji na tija katika kilimo.
Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki mwaka huu yanatarajiwa kufanyika katika viwanja vya maonesho mkoani Morogoro kuanzia 1 hadi 8 Agosti 2025, yakihusisha mikoa ya Tanga, Pwani, Dar es Salaam na Morogoro.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa