Leo tarehe 1 Agosti 2025 , Wananchi mbalimbali wameendelea kujitokeza kwa wingi katika banda la Halmashauri ya Wilaya ya Pangani katika viwanja vya maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki, Mkoani Morogoro ambapo wamepata elimu ya namna bora ya kilimo cha ndizi.
Wataalam wa kilimo kutoka Halmashauri hiyo waliwaelekeza wananchi kuhusu mbinu sahihi za uchaguzi wa miche, maandalizi ya shamba, utunzaji wa mashina, udhibiti wa magonjwa na wadudu pamoja na njia bora za kuongeza uzalishaji wa zao hilo.
Elimu hii inalenga kuwawezesha wakulima kuongeza tija na ubora wa mazao ya ndizi, ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali kuboresha sekta ya kilimo na kukuza uchumi wa kaya kupitia maonesho ya Nane Nane mwaka huu yenye
Kauli mbiu: "Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
2025."
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa