Mtendaji wa kijiji cha Mtango akishirikiana na wataalam mbalimbali kutoka ofisi ya kata Mikinguni pamoja na wataalam wa Afya kutoka Zahanati ya kijiji cha Mtango wameshiriki katika maadhimisho hayo ambapo shughuli mbalimbali zimefanyika ikiwemo; ugawaji wa Vyandarua kwa akina mama wajawazito ,Kufanya tathimini ya hali ya Lishe kwa Watoto chini ya miaka mitano ,na kutoa matone ya Vitamin A (routine)
Maadhimisho hayo yamefanyika Septemba 1,2023 katika Zahanati ya Mtonga iliopo kijiji cha Mtonga Wilayani Pangani.
Jumla ya watoto waliofanyiwa tathimini ya hali ya Lishe kwa kipimo cha MUAC ni Watoto 61 (21Me, 40Ke) ambapo hali zao za Lishe iko vizuri kwamaana ya kijani .
Aidha wataalamu hao wameendelea kutoa wito kwa wazazi kuendelea kuwapatia watoto vyakula mchanganyiko ili kukidhi maana ya Lishe bora na hatimaye kuchangia katika kuondoa hali ya utapiamlo na udumavu katika kaya na hatimaye kuimarisha hali ya Lishe kwa watoto
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa