Halmashauri ya Wilaya ya Pangani kupitia idara ya kilimo mifugo na uvuvi inaendelea na jitihada za kuingiza zao la alizeti kama zao la biashara katika Wilaya hiyo.
Katika kutekeleza juhudi hizo, tayari vikundi mbalimbali vinatekeleza kwa vitendo juhudi hizo.
Miongoni mwa vikundi hivyo ni pamoja na kikundi cha kilimo mseto kinacho tekeleza mradi wa kiwanda kidogo cha kusindika zao hilo la alizeti kilichopo katika kijiji cha Mbulizaga Wilayani Pangani, pamoja na kiwanda kidogo cha Veronica Swai mkazi wa kijiji cha Sakura.
Wakizungumza mala baada ya kutembelewa na maafisa kilimo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, wanakikundi hao wamebainisha faida mbalimbali wanazopata kutokana na viwanda hivyo vidogo vya kusindika zao hilo, na kumshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya kilimo ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa pembe jeo na mbegu bora kwa wakulima.
Ikumbukwe kuwa kiwanda hiki kidogo cha kusindika zao la alizeti kilichopo kijiji cha Mbulizaga, kilizinduliwa na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru ndg Charles Francis Kabeho tarehe 10/10/2018.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa