MAADHIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA.
Pangani -Tanga
Leo tarehe 5 .12.2024 Mhe,Juliana kibonde mkurugenzi Idara ya maendeleo ya jinsia kutoka wizara ya maendeleo ya Jamii,jinsia wanawake na makundi maalum amesema ni jukumu la Jamii nzima kutoa taarifa kupinga ukatili wa kijinsia.
Ameyasema hayo alipokua katika Kijiji Cha Bweni Wilaya ya Pangani katika maadhimisho ya siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia yaliyo hudhuriwa na taasisi mbalimbali za kupinga ukatili wa kijinsia.
Kwa upande mwingine viongozi wa dini wamekemea vikali vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia Kwa wanawake na kuwataka wazazi kuwaangalia vyema watoto wao katika malezi Yao .
Nae Ramadhani shabani mmoja wa wasanii ambao wameshiriki katika shughuli hii ya kupinga ukatili wa kijinsia amesema umefika wakati sasa wa Jamii kubadilika na kuachana na vitendo hivi vya ukatilia wa kijinsia .
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali ,Taasisi 26 ikiwemo UZIKWASA zinazopinga maswala haya ya ukatili wa kijinsia,wasanii na wananchi wa Kijiji hicho Cha Bweni.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa