Tarehe 19/09/2025, wakazi wa Kipumbwi waliungana kwenye viwanja vya kijiji kuadhimisha Siku ya Afya na Lishe. Jumla ya watu wazima 79 (wanaume 46 na wanawake 33) walihudhuria.

Shughuli kuu zilizofanyika:Elimu ya lishe kwa kutumia meza ya chakula ,Mapishi ya uji wa lishe mchanganyiko, Upimaji wa afya (uzito, urefu, shinikizo la damu, sukari, MUAC kwa watoto, na huduma za HIV)

Aidha limefanyika Igizo na shairi kuhusu lishe, afya ya mama na mtoto, na mabadiliko ya tabianchi
Watoto 133 walipimwa lishe kwa kipimo cha MUAC na wote walionekana kuwa na hali nzuri ya lishe.

Tunawashukuru sana Afisa Lishe na timu yake kwa uongozi na kujitoa katika kufanikisha siku hii muhimu kwa jamii yetu ya Kipumbwi.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa