Bi Heliswida Majula Afisa Tarafa wa Pangani Mjini ambae amemuwakilisha Mkuu wa Wilaya mhe Zainab Abdallah amesema kuwa hali ya maambukizi ni asilimia 5 hivyo ameiomba jamii kuendelea kupambana na maambukizi hadi kufikisha asilimia 0 ya maambukizi ya Ukimwi,Wilayani Pangani.
Ameongeza kuwa tunashauriwa kupima kila baada ya miezi mitatu ili kuweza kujua Afya yako na kwa wale ambao watakutwa na maambukizi waweze kutumia dawa pasipo kuacha.
"Sote tumeona kwa wale ambao wanatumia dawa kwa uaminifu wamefanikiwa kufubaza makali ya virusi na kuendelea kuongeza nguvu kazi ya jamii".
Hata hivyo ametoa wito kwa jamii kuacha kuwaambukiza wengine kwa makusudi, na Wananchi kutoendeleza ngono zembe na Elimu ya matumizi ya kinga iendelee kutolewa kwa ngazi zote ili kupambana na janga hili.
Hata hivyo amezipongeza taasisi zote zinazotoa Elimu kwaajili ya kujikinga na maambukizi ya Ukimwi ikiwemo Uzikwasa,Pangani fm, lenga mbali na taasisi zote zinazosaidia kupaza sauti ya kupambana na Maambukizi ya Ukimwi.
#panganibilaukimwiinawezekana
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa