Maafisa Bajeti wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani wamepatiwa mafunzo ya Maandalizi ya Mpango na Bajeti pamoja na Mafunzo ya Mfumo wa PLANREP kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 yaliyoandaliwa na Idara ya Mipango, Uratibu na Ufuatiliaji.
Mafunzo hayo yamefanyika leo Ijumaa tarehe 5 Januari, 2024 katika ukumbi wa Zamani wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani.
Akifungua mafunzo hayo Mkuu wa Idara ya Mipango Uratibu na Ufuatiliaji ndg SIMEON VEDASTUS MZEE amewataka Maafisa Bajeti wote kuandaa Bajeti zao kwa makini kwa Mwaka wa fedha 2024/2025 ili kuepuka changamoto zinazojitokeza kwenye utekelezaji wa Bajeti hizo.
"Ni muhimu kila Idara iweze kupitia Muongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 ili kuepuka changamoto ifikapo wakati wa utekelezaji wa Bajeti hizo".
Ameongeza kuwa kwa yale maeneo yote muhimu kwenye Bajeti zetu yanapaswa kutengewa Fedha za kutosha ili yaweze kukamilisha mahitaji yake kwa mwaka wa fedha husika.
Maafisa Bajeti katika Mafunzo hayo wamepata nafasi ya kupitia Mpango na Bajeti za Idara ya Afya na Elimu kwa Mwaka 2024/2025, Matumizi ya mfumo wa Bajeti(Planrep), Mafunzo kwa Vitendo mfumo wa Planrep pamoja na kupatiwa Username na Password za Planrep kwa kila Idara na Kitengo.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa