Maafisa Ugani Pangani wakabidhiwa Pikipiki
Katibu Tawala Wilaya ya Pangani bi Ester Gama leo tarehe 09 Oktoba , 2024 amekabidhi pikipiki aina ya Boxer Kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Pangani Mhe. Gift Isaya Msuya zilizotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa Maafisa Ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani ambazo zitarahisisha utendaji kazi.
Akikabidhi pikipiki hizo Bi Ester Gama amewataka kwenda kuzitunza na kuzifanyia kazi iliyokusudiwa ambapo amesema pikipiki hizo zitawasaidia kurahisisha usafiri katika maeneo yao ya kazi ikiwa ni jitihada ya kuhakikisha wanawafikia wafugaji na kutatua changamoto zinazowakabili.
"Pikipiki hizi zikafanye kazi iliyokusudiwa ambayo ni kuwafikia wakulima kwenye maeneo yao na kutatua changamoto mbalimbali za wananchi". Amesema.
Kwa upande wao Maafisa Ugani hao wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha mazingira ya kufanyia kazi.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa