Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Ndg Ramadhani Zuberi( Mwenye Shati jekundu), amezindua zoezi la ugawaji wa pikipiki zilizotolewa na Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Zoezi hilo limefanyika leo Jumatatu Disemba 4, 2023, katika ofisi ya Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Pangani.
Akizindua ugawaji wa pikipiki 3 aina ya Boxer zenye namba za usajili STM 7261,7262 na 7263 zilizotolewa kwa Maafisa Ugani Sekta ya Mifugo, Ndg. Ramadhani Zuberi amewataka Maafisa ugani hao kuzitumia pikipiki hizo kwa shughuli ya kuihudumia jamii na si vyinginevyo. Amesisitiza kuwa upatikanaji wa pikipiki hizo uendane na matokeo chanya kwa jamii.
Ndg. Ramadhani Zuberi amewaasa pia Maafisa hao kutumia pikipiki hizo kwa umakini na tahadhali ili kujilinda na ajali ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya wataalam wa Serikali.
Akizungumza kwa niaba ya Maafisa ugani, bwa Elisha Katani ameishukuru ofisi ya Mkurugenzi chini ya bwan Isaya M Mbenje pamoja na Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutatua changamoto ya Maafisa ugani katika utoaji wa huduma kwa Jamii. Amesema kupitia Pikipiki hizi Jamii itapata huduma kwa wakati Kwa kuwa uwezo wa kuwafikia umeimarishwa.
Pikipiki hizo zinatolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya kiongozi Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na huu ni mwendelezo wa kuimarisha mazingira ya wataalam katika kuwahudumia wananchi kwa wakati na uhakika.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa