Timu ya madaktari Bingwa wa Rais Samia wamewasili ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani mapema leo tarehe 21 Oktoba 2024 kwaajili ya kutoa huduma za Kibingwa ndani ya Hospitali ya Wilaya.
Miongoni mwa Madaktari hao ni pamoja na Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake na ukunga, Daktari bingwa wa watoto na watoto wachanga, Daktari bingwa wa upasuaji na mfumo wa mkojo, Daktari bingwa wa usingizi na ganzi,magonjwa ya ndani, Daktari bingwa wa kinywa na meno pamoja na Daktari bingwa wa mifupa na ajali.
Huduma zote zitatolewa kuanzia tarehe 21 hadi 26 Oktoba 2024 kuanzia saa mbili kamili asubuhi ndani ya Hospitali ya Wilaya ya Pangani.
" Madaktari bingwa wa Rais Samia , Tumefika karibu tukuhudumie".
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa