Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Mhe. Gift Isaya Msuya, amefungua mafunzo maalumu ya Uraia na Utawala Bora kwa Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Mafunzo haya, yaliyofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya leo tarehe 17 Machi 2025, yameandaliwa na Wizara ya Katiba na Sheria.
Mhe. Msuya aliwashauri watumishi wa umma kuzingatia mafunzo hayo ili kuboresha utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku na kuhakikisha huduma bora kwa wananchi.
Aidha, mratibu kutoka ofisi ya Katiba na Sheria alielezea kuwa lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo watumishi kuhusu haki na wajibu wao kikatiba, pamoja na kuwasaidia viongozi wa Serikali za Mitaa kukuza uzalendo na kutoa huduma bora.
Mhe. Msuya pia alisisitiza umuhimu wa usimamizi mzuri wa ulinzi na usalama, akisema kuwa watendaji wa umma wanapaswa kushirikiana kuhakikisha changamoto za maeneo yao zinatatuliwa na kuondoa madhara kwa wananchi.
Alifafanua kuwa Serikali ina jukumu la kulinda wananchi na kuhakikisha amani na usalama vinadumishwa ili kuleta manufaa chanya kwa jamii.
Kwa ujumla, mafunzo haya ni muhimu katika kukuza utawala bora na kutoa huduma za kisasa na bora kwa wananchi.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa