Leo tarehe 22 Septemba 2025, mashindano ya Ardhi Tanga Super Cup yamehitimishwa kwa shamrashamra kubwa, viwanja vya Jaira Wilayani Pangani.
Aidha katika mchezo wa fainali, kwa mpira wa miguu timu ya Madanga FC imeibuka bingwa baada ya kuifunga timu ya Mivumoni FC goli 2 – 0 na kuondoka na jezi, mpira na kombe la heshima.
Kwa upande wa mpira wa pete, Mwembeni wameonyesha ubabe kwa kuwashinda Kigurusimba na kubeba zawadi za jezi, mipira na majiko ya gesi.
Mashindano haya yamewezeshwa na World Vision Tanzania yakibeba ujumbe muhimu wa Kuhamasisha utunzaji wa mazingira pamoja na Kukuza matumizi ya nishati safi ya kup
ikia.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa