Halmashauri ya Wilaya ya Pangani leo 26 Juni,2023 imepokea Timu ya watalaamu kutoka Wizara ya kilimo kutoa mafunzo elekezi kwa vijana wa Pangani.
Timu hiyo imefanikiwa kushiriki kikao kilicho hudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bi Zainab Abdallah,Kamati ya Ulinzi na usalama Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Bw. Isaya M Mbenje,Waheshimiwa Madiwani wa kata zote, Katibu Tawala wa Wilaya,Viongozi wa Chama cha Mapinduzi, pamoja na Wakuu wa Idara na vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani
Mafunzo hayo pia yatahusisha namna bora ya kuwekeza kwenye kilimo cha kisasa.
Akizungumza na Viongozi wa Wilaya na Halmashauri hiyo kwenye Kikao, Mkuu wa msafara wa Timu hiyo Ali Hemed alisema mafunzo kwa vijana yatawezesha kupata ujuzi wa kilimo bora na kwa tija zaidi.
"Tutawezesha vijana kupima aina ya udongo na kutambua ni aina gani ya mazao wanayoweza kujihusisha nayo kwa vipindi vyote vya mwaka bila kuathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi" alisisitiza zaidi Hemed.
Amesema kuwa vipaumbele ni mazao ya nafaka kama vile mahindi, mpunga ambayo mavuno yake ni kila baada ya miezi sita.
Mkuu wa Wilaya ya Pangani Mhe. Zainab Abdallah ameipongeza Wizara na kutoa wito kwa wananchi wa Pangani kushirikiana na Waataalamu hao kuleta maendeleo ya kisasa katika Kilimo
" Tunataka Wilaya ya Pangani iwe chanzo ama kapu la kulisha mikoa ya Tanga, Dar es salaam pamoja na jirani yetu Zanzibar" alisema Zainab
#pangani yetu
#kazi iendelee.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa