Kuelekea maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanganyika, wananchi Halmashauri ya Wilaya ya Pangani wamekiri kuwepo mafanikio makubwa katika sekta za elimu na afya, yaliyotokana na juhudi za Serikali.
Wananchi hao wamedhibitisha hayo, wakati wa Mdahalo maalum uliowashirikisha wakazi wa halmashauri ya Pangani uliojadiri "Miaka 62 ya Uhuru, tulipotoka, tulipo na tunapoelekea".
Mdahalo huo uliongozwa na wananchi wamebainisha matokeo ya mapambano dhidi ya ujinga yanayojidhihirisha wazi, kutokana na ongezeko la wasomi lililotokana na uwepo wa shule na vyuo vya kati na vikuu katika mikoa yote nchini, uliotoa fursa ya kila mtanzania kupata elimu.
"Kwa sasa Serikali imetoa fursa kila mtanzania kuwa na haki ya kupata elimu, kuanzia elimu ya awali mpaka chuo kikuu, tofauti kabla ya Uhuru elimu ilitolewa kwa ubaguzi, kubwa zaidi uwepo wa shule za serikali kila kata, za mashirika na binafsi kwa ujumla zimepanua wigo wa wananchi kuondokana na ujinga".
Mzee Sekibaha amezungumzia hali halisi ya mabadiliko katika sekta ya usafiri na usafirishaji, watanzania wakiwa wanajivunia maendeleo ya miundombinu ya barabara zinazofikika.
" katika Wilaya yetu tuna raha sisi wana pangani, barabara yetu inapitika".
Kwa upande wake bw Athuman Ally maarufu kama mzee Pwagu amezungumzia mabadiliko makubwa katika mji wetu wa Pangani.
"Maendeleo ya zamani na sasa ni tofauti, kwa sasa sote tunajionea vijana wetu wanasoma vizuri, hospitali pia tumepatiwa". Tunawashukuru viongozi wetu mbunge wetu Jumaa Aweso pamoja na Mkuu wetu wa Wilaya bi Zainab Abdalla, na tuko pamoja na viongozi wetu wote katika Wilaya yetu.
Serikali imefanikiwa kuboresha sekta ya afya kwa kusogeza huduma za afya, karibu na wananchi kwa kuhakikisha kila Tarafa inakuwa na kituo cha afya.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa