Milioni 128 zawasaidia wasichana 80 wenye mahitaji maalumu Shule ya Msingi Funguni.
Hayo yamebainishwa Julai 17,2024 wakati wa ziara ya Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango kukagua ujenzi wa jengo la Bweni la Wanafunzi wenye mahitaji maalum shule ya Msingi Funguni.
Akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya mradi huo bi Flora Mayaka amesema kuwa
" Tunatoa shukrani zetu kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha shilingi milioni 128 kwaajili ya mradi mkubwa wa ujenzi wa bweni la Wanafunzi wenye mahitaji maalum, kitengo cha akili katika Shule hii". Alisema.
Hadi sasa ujenzi huu bado unaendelea na utakapo kamilika unatatarajia kusaidia jumla ya wanafunzi 80 wenye mahitaji maalum.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa