Ukarabati wa Soko Kuu la Pangani ulioanza tarehe 15.01.2023, na kugharimu takribani shilingi Milioni,(87,397,763) umefika tamati na kutoa jawabu la kudumu kwa wafanya biashara 40 wakiwamo wafanya biashara 31 wa Vizimba,wafanya biashara 4 wa Mabucha pamoja na wafanya biashara 5 wa Fremu za maduka.
Ameyasema hayo leo tarehe 05.07.2023, Afisa biashara wa halmashauri ya wilaya ya Pangani .Bi Jenipha A Nyahongo wakati akiongoza zoezi maalumu la ugawaji wa Vizimba pamoja na Fremu za Maduka kwa wafanya biashara wa soko hilo.
Ikumbukwe kuwa Soko Kuu la Pangani limekarabatiwa kutokana na Mapato ya ndani ya Halmashauri pamoja na mchango kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga,Ndugu Rajabu Abdu Rrahman Ametoa milioni 5 na Mheshimiwa Mbunge wa Pangani Juma Hamidu Aweso ambae ametoa milioni 10 ili kuunga mkono ukarabati huo.
Mwenyekiti wa Soko hilo Mzee Said Athuman Goroto ameishukuru Serikali kwa niaba ya Wafanya Biashara na kuahidi kulitunza soko hilo kwani limekuwa ni sehemu kubwa ya utendaji kazi bora na kwa manufaa ya vizazi vyao.
Ukarabati wa soko hilo ni miongoni mwa miradi iliyozinduliwa na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru ndugu Abdalla Shaib Kaim
#pangani yetu
#kazi iendelee
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa