Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Ndg. Charles Edward Fussi (katikati), amekutana na kuwaaga rasmi watumishi wachezaji wa Timu ya Halmashauri wanaotarajia kuelekea jijini Tanga kushiriki Mashindano ya Shirikisho la Michezo kwa Serikali za Mitaa (SHIMISEMITA) yatakayofanyika kuanzia Agosti 15 hadi 29, 2025.
Hafla hiyo imefanyika leo 13 Agosti 2025 katika ukumbi wa Halmashauri Mkoma, ambapo Mkurugenzi amewataka wachezaji kujitoa kikamilifu, kushirikiana na kuhakikisha ushindi unapatikana ili kuipatia heshima Halmashauri ya Wilaya ya Pangani.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni:
"Jitokeze Kupiga Kura, kwa Maendeleo ya Michezo".
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa