Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Bw. Charles Edward Fussi, amewataka watumishi wapya waliopata ajira katika Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kufanya kazi kwa uadilifu, kujituma na weledi mkubwa ili kuleta maendeleo na kuwahudumia wananchi kwa ufanisi.

Akizungumza na watumishi hao leo tarehe 28 Julai 2025 katika ofisi yake iliyopo Mkoma, Bw. Fussi amesema Serikali imewekeza rasilimali nyingi kuajiri wataalamu hao, hivyo ni jukumu lao kuhakikisha wanakuwa chachu ya maendeleo hususan katika sekta za uzalishaji.

“Mmekuja kusaidia wananchi, si kwa maneno bali kwa matendo. Hakikisheni mnafika kwa wakulima, wafugaji na wavuvi, kusikiliza changamoto zao na kutoa suluhisho la kitaalamu,” alisema.
Aidha, aliwataka kuwa mfano wa kuigwa katika nidhamu ya kazi, kuheshimu taratibu za utumishi wa umma na kushirikiana na watumishi waliowakuta kazini kwa ajili ya kujifunza zaidi.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa