Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Isaya M Mbenje amempongeza Mkuu wa Wilaya Mhe Zainab Abdallah kwa kufungua Maonyesho ya Wafanya Biashara Pangani.
Ametoa pongezi hizo leo Septemba, 19, 2023, wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya Wafanya Biashara katika Wilaya hio.
" Sisi hapa tunajaribu kutengeneza historia bora ya Wilaya ya Pangani na jambo hili mkuu wetu analisimamia tunajenga misingi imara hivyo nawaomba wananchi wa Pangani tuje kujifunza na kuunga mkono juhudi hizi".
Pia amewaomba wanapangani wazidi kualika watu mbalimbali ili kuifikia fursa hii ya Biashara hapa Pangani na kuendelea kuwakaribisha wawekezaji wa ngazi zote kuwekeza hapa Pangani
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Pangani mhe Akida Bahorera amepongeza juhudi hizi za Mkuu wa Wilaya mhe Zainab Abdallah na kuongeza kuwa sasa ni wakati sahihi wa kuitoa Pangani shimoni na kupaa angani.
Lengo la Maonyesho haya ya biashara ni kuwaunganisha Wajasiriamali na Wafanya Biashara kutoka maeneo mbalimbali nchini na kutangaza bidhaa zao.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa