Halmashauri ya Wilaya ya Pangani leo Tarehe 02.02.2024 imefanya Mkutano wa Baraza la Halmashauri hiyo katika ukumbi wa zamani wa Halmashauri kwa kipindi cha robo ya Pili Oktoba hadi Disemba kwa mwaka wa Fedha 2023/2024 ikiwa ni kuwasilisha taarifa kutoka katika Kata 14 zilizopo katika Halmashauri hiyo.
Aidha Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani ndg Juma Mbwela amewakalibisha Waheshimiwa madiwani pamoja na Wataalamu wote na kumuomba Mwenyekiti wa Halmashauri kufungua mkutano huo.
Akifungua mkutano huo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani mhe Akida Bahorera amewataka waheshimiwa Madiwani kujadili taarifa zote kwa weledi na kutoa michango yao ili waweze kufikia malengo.
Waheshimiwa Madiwani wamewasilisha taarifa za utendaji kazi wa Kata zao na kueleza hali ya utoaji wa hudumu za kijamii kwa ujumla na utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo, Masuala ya Elimu katika Kata, hali ya shughuli za kiuchumi, mafanikio, changamoto na utatuzi wake, utunzaj wa mazingira.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Mkwaja mhe Dhafa H Jumbe ameishukuru Serikali kupitia Tanesco kwa kuingiza Umeme katika Shule ya Sekondari Mkwaja kwani jambo hilo limekuwa msaada mkubwa kwa Wanafunzi wa Shule hiyo.
#panganimpya
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa