Leo Disemba 11,2023 wajumbe wa kamati ya Siasa Wilaya ya Pangani chini ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya CDE Abdallah M Abdallah wamefanya ziara na kukagua mradi wa Miji 28, unaotekelezwa, Boza Wilayani Pangani.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa Mradi huo wa Miji 28 mhandisi bwa. Salim Ngumba amefafanua kuwa-"
"Mtekelezaji wa programu hii ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan ambayo imetoa jukumu hilo kwa wizara ya maji katika mkoa wa Tanga".chini ya mhandisi mshauri WAPCOS LTD na Mkandarasi ambae ni JWIL INFRA LTD.
Ameongeza kuwa mradi huu wa Maji utanufaisha Wilaya Nne (4), zikiwemo Handeni, Muheza,Korogwe pamoja na Pangani.
Akiongea mala baada ya upokeaji wa Taarifa hiyo Mkuu wa Wilaya ya Pangani mhe Zainab Abdallah amesema kuwa anaishukuru Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani Mradi huu wa kimkakati umesanifiwa ili kuongeza hali ya upatikanaji wa Maji Safi na Salama katika Miji ya Pangani, Muheza, Korogwe na Handeni. Amewataka wakandarasi kukamilisha mradi huo kwa wakati.
Mhe Zainab Abdallah ameongeza kuwa-"
"Niendelee kumshukuru Waziri wa Maji mhe Jumaa Aweso kwa kuendelea kuipigania Wilaya yetu ya Pangani hasa katika miradi hii ya maendeleo".
Aidha kwa upande wake Mwenyekiti wa Ccm Wilaya ya Pangani Cde Abdallah amesema anaipongeza Serikali kwa kuiwezesha Pangani Fedha za mradi huu kwani utakapokamilika utatoa fursa za upatikanaji wa maji safi na salama kwa masaa yote 24.
Aidha wakandarasi wameahidi kukamilisha Mradi huu ifikapo Disemba 2024.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa