Hayo yamethibitishwa leo tarehe 14 juni 2025, wakati Mwenge wa Uhuru ulipotembelea na kuridhishwa na utekelezaji wa mradi huo na kupelekea kuwekwa jiwe la Msingi.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani bi Sophia amesema kuwa " Ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Mwembeni ulianza kutekelezwa mnamo tarehe 19 Februari, 2024 kupitia Halmashauri, wananchi wa kijiji cha Mwembeni na Wadau mbalimbali wa maendeleo". Alisema
Aidha aliongeza kuwa Hadi kufikia tarehe 13 Mei, 2025 vimepokelewa vifaa na fedha taslimu zenye jumla ya Shilingi Milioni 80,956,900.00 katika mradi huu ambapo zinajumuisha fedha kutoka Mapato ya ndani ya Halmashauri, fedha na vifaa toka Wadau mbalimbali, vifaa toka Mfuko wa Jimbo na nguvu za wananchi zimetumika kutekeleza mradi huu.
Akiongea mala baada ya kupokea taarifa hiyo, kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa ndg Ismail Ali Usi amesema kwa kweli wananchi wa Mwembeni wameonyesha uzalendo kwa kuupokea Mwenge wa Uhuru.
" Tunajionea faraja kwa kuona wananchi wanaenda kupata huduma bora kwa miundombinu hii ya afya, na hii ni ahadi ya Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha anaendelea kuboresha miundombinu ya afya katika maeneo yetu " Alisisitiza.
Sambamba na hilo Halmashauri ya Wilaya ya Pangani inatoa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna ya pekee anayoendelea kuboresha Huduma za afya katika Wilaya yetu kwa upande wa miundombinu, dawa na vifaa tiba. Aidha, wadau wote na wananchi wa Mwembeni kwa michango yao ya hali na mali katika ujenzi wa zahanati hii.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa