Mwenge wa Uhuru umekagua na kuzindua mradi wa Ujenzi wa jengo la Radio Pangani Fm 107.5 lililopo Boza Wilayani Pangani.
Hayo yamefanyika leo Aprili 16,2024 ,Mwenge wa Uhuru ulipotembelea na kukagua mradi huo.
Akiwasilisha taarifa ya mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi hiyo ya kiraia ndugu Novatus Urassa amesema kuwa Pangani Fm Radio inayomilikiwa na asasi ya UZIKWASA ina lengo la kuwasaidia viongozi na wananchi kuwasiliana juu ya masuala mbalimbali ya kimaendeleo.
"Tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuweka Mazingira rafiki yanayowezesh a asasi za kiraia ikiwemo asasi hii kutekeleza majukumu yake ndani ya Nchi yetu ".
Akizungumza mala baada ya ukaguzi wa mradi huo kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa ndugu Godfrey Mnzava amesema kuwa_:
"Tunawapongeza sana watu hawa kwani hata TRA wameendelea kuwatambua katika ulipaji wa mapato, hivyo Mwenge wa Uhuru upo tayari kwa ufunguzi wa jengo hili".
Bwan Urassa ameongeza kuwa hadi sasa mradi huu umegharimu Shilingi milioni 777 fedha zilizotokana na wafadhiri ( Bread for the World kutoka Ujerumani) na kubainisha kuwa hadi sasa Pangani Fm Radio imetoa ajira za kudumu 33 ambapo wakike 14 na Wakiume 19.
Radio hii inatoa fursa kwa wananchi wa Pangani na maeneo jilani kupata habari mbalimbali zilopo ndani na nje ya nchi.
# "Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu".#
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa