"Mimi kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara nimefarijika sana kuwa mgeni rasmi wa kongamano hili na kueleza mikakati ya Serikali katika kuendeleza Biashara na Uwekezaji hapa Pangani".
Hayo yamesemwa Jumanne ,Oktoba 3 , 2023, na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Silaoneka Kigahe, wakati wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji.
Aida Mhe Kigahe ameongeza kuwa makongamano haya yanafaida mbalimbali ikiwemo kutoa fursa ya kujadiri fursa mbalimbali za uwekezaji.
"Ili tuweze kuendelea lazima tuifungue Pangani kwa kuendelea kuzichangamkia fursa za biashara zinazopatikana katika Wilaya hij ya Pangani hasa kwa wawekezaji wa ndani pamoja na wa Nje kwa manufaa ya Taifa letu na uchumi kwa ujumla, ili kutoa majawabu ya fursa zinazopatikana ili wananchi waweze kunufaika nazo".
Ameongeza kuwa , "tunapaswa kuyaandaa maeneo yetu ya uwekezaji na tuepuke yasiwe maeneo yenye migogoro, lengo letu kama Nchi ni kuona mali gafi zote za Tanzania zinaenda kuongezwa thamani, ili tupate malighafi zenye ubora zaidi".
Lengo letu tupate Bandari ya kusafirisha bidhaa za mwisho na sio kuuza malighafi, na tuendelee kuboresha na kauli mbiu yetu iwe Pangani ni mahali salama ya uwekezaji.
Tumeona ipo haja sasa ya kuwaleta wawekezaji kuja kuongeza thamani ya bidhaa zetu, Pangani bado haijatumika,naendelea kumpongeza mkuu wa Wilaya hii kwa kuwa mstari wa mbele kufanya kitu cha tofauti.
Hata ivyo ameziomba Taasisi zote zikiwemo SIDO,TBS, BLERA,zifike kwenye ngazi za Halmashauri ili ziweze kutoa huduma kwa Wananchi wa ngazi za chini.
#Panganimpya
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa