Leo Tarehe 23 Septemba 2024 ,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani kupitia Idara ya huduma za Afya ,Ustawi wa jamii na Lishe, Kwa kutumia wataalam wa Lishe imeendesha zoezi maalum la huduma mkoba yenye lengo la kufanya tathimini ya hali ya Lishe( BMI Assessment)
Zoezi hilo limehusisha watumishi wanaofanya kazi katika taasisi zote za kiserikali zilizopo ndani ya Halmashauri kama njia ya kupambana na magonjwa yasiyo ambukiza, ambapo leo watumishi wanaofanya kazi katika taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wamepatiwa huduma hiyo.
Aidha ,Programu hii inaendeshwa kwa kauli mbiu isemayo" Utumishi ni dili, Zingatia unachokula " ikiwa na lengo la kuhamasisha mabadiliko chanya ya ulaji na mfumo wa maisha kwa watumishi.
Programu hii maalumu inatarajiwa kuhitimishwa tarehe 27/09/2024.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa