Ofisi ya Udhibiti Ubora wa Shule na Idara ya Elimu Msingi, Wilaya ya Pangani, wametoa mafunzo wezeshi juu ya Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu kwa Shule za Awali na Msingi.
Moja ya Mafunzo hayo yametolewa leo Januari 11, 2024 katika kituo cha Walimu (TRC Pangani) ambapo Elimu juu ya Mtaala ulioboreshwa kwa Walimu Wa Shule za Msingi,na Awali imetolewa kwa Walimu hao.
Akiwasilisha taarifa ya Mtaala huo, Afisa Elimu Kata ndg Mbaga Musa amesema kuwa moja ya maboresho yaliyofanywa katika mtaala ulioboreshwa ni pamoja na kubainisha sifa mbalimbali za walimu wanaopaswa kufundisha Shule za Awali na Msingi, pamoja na Utekelezaji wa Waraka huo.
Kwa upande wake ndg Frank Maeda kutoka Ofisi ya Udhibiti Ubora wa Shule Wilaya ya Pangani, amesema kuwa miongoni mwa mambo muhimu yanayo paswa kufundishwa ni pamoja na Uzalendo, Utamaduni, Masuala Mtambuka pamoja na Elimu ya Imani.
" Wanafunzi wajengwe katika imani zao na kufundishwa Tunu za Taifa ikiwa ni pamoja na Uhuru, Amani,Mshikamano pamoja na Upendo kama mtaala huu ulioboreshwa unavyoeleza.
Aidha kwa upande wake ndg. Faraji Ally Mwalimu wa Shule ya Msingi Pangani, amesema kuwa mafunzo haya ni fursa bora kwa sisi walimu, kwani yanatujenga katika uboreshaji wa utoaji maarifa kwa wanafunzi wetu, hivyo ni mafunzo muhimu kwetu kwa manufaa ya Taifa letu.
Ikumbukwe kuwa Uboreshaji wa Mtaala huu umeanza kutumika kutoka Tarehe 9 Disemba 2023.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa