Halmashauri ya Wilaya ya Pangani imefanya kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi PHC (Primary Health Care) ) kwaajili ya kutambulisha mradi wa huduma endelevu ya maji na usafi wa mazingira Vijijini.
Kikao hicho kimefanyika leo Disemba 22,2023 katika ukumbi wa Zamani wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani.
Kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Katibu Tawala Wilaya hiyo, ndg Ester Gama amefungua kikao hicho na kutoa rai kwa Wananchi kuendelea kuhamasisha jamii ili waweze kujitoa kwa nguvu zote katika kukamilisha miradi hio yenye faida kubwa kwa Halmashauri na Wananchi kwa ujumla.
Aidha wajumbe mbalimbali wamehudhulia ikiwemo kamati ya ulinzi na usalama Wilaya, Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu na Afya mhe Akida Bora Mimi, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Pangani ndg Veronica Marwa, na Wataalam wengine ambao wameshiriki ili kujadiliana namna bora ya utekelezaji wa Mradi huo.
Katika Uwasilishaji wa taarifa ya Mradi huo Afisa Afya kutoka Ofisi ya Mganga mkuu Wilaya ya Pangani ndg Revocatus Asseys meeleza kuwa, Mradi huo unatekelezwa kwa kuzingatia viashiria mbalimbali kwa idara ya Afya na Elimu, miongoni mwa viashiria hivyo ni pamoja na Matumizi ya Vyoo bora, idadi ya Shule zenye vyoo bora,idadi ya Vijiji vilivyofikia daraja la juu la usafi wa Mazingira.
Ameongeza kuwa hadi Disemba 21,2023 katika vituo vyote miradi ipo hatua za ujenzi na kazi zinaendelea.
Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi ndg Veronica Marwa amesema kuwa hadi sasa fedha za miradi hii zimeshapokelewa na utekelezaji wa miradi unaendelea, na ameeleza kuwa kiuhalisia vituo vyetu vya huduma za Afaya vinahitaji kuboreshwa zaidi na Serikali imeendelea kutupatia fedha za miradi na uboreshaji wa mazingira ya Afya unafanyika.
#panganimpya
#kaziiendelee.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa