Leo tarehe 02 Oktoba 2025, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, ambaye pia ni Mhasibu Ndugu Piusi Mmasi, amefungua rasmi mafunzo ya siku mbili kwa Maafisa Bajeti wa Idara na Vitengo katika ukumbi wa TRC.
Aidha, mafunzo hayo yatawawezesha Maafisa Bajeti kuhakikisha maandalizi, usimamizi na ufuatiliaji wa utekelezaji wa mipango na bajeti unafanyika.
Akizungumza wakati wa ufunguzi, Ndugu Pius Mmasi amewataka washiriki wote kuwa makini na kutumia mafunzo hayo ipasavyo kwa manufaa ya wananchi wa Pangani.
Sambamba na hilo ndugu Emmanuel Mbonde Afisa mipango amefafanua kuwa "Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo washiriki katika uandaaji wa bajeti kupitia mfumo wa PlanRep, ili kuhakikisha mipango ya maendeleo ya Halmashauri inatekelezwa kwa ufanisi". Alisema.
Hatua hii ni mwanzo rasmi wa mchakato wa awali wa maandalizi ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027 ya Halmashauri ya Wilaya y
a Pangani.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa