Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Mheshimiwa Gift Isaya Msuya, anawaalika na kuwasihi wananchi wote wa Wilaya ya Pangani kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mapokezi na mbio za Mwenge wa Uhuru zitakazofanyika tarehe 14 Juni 2025 katika viwanja vya Shule ya Msingi Mwembeni.
Ametoa rai hiyo leo juni 14, 2025, ambapo amebainisha kuwa ziara hiyo, Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Zahanati ya Mwembeni, Nyumba ya Wakuu wa Idara Mkoma, Shule Mpya ya Sekondari ya Muhembo,ukarabati wa barabara ya Mnyongeni na utatumika kukagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa manufaa ya wananchi.
Mheshimiwa Msuya amesisitiza kuwa Mwenge wa Uhuru ni alama ya umoja, mshikamano na maendeleo, hivyo ni fursa muhimu kwa wananchi kuonesha uzalendo na mshikamano katika kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Wananchi wote wanahimizwa kujitokeza kwa wingi na kwa wakati ili kushiriki kikamilifu katika shughuli hiyo muhimu kwa maendeleo ya Taifa.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa