Halmashauri ya Wilaya ya Pangani inatarajia kuanza rasmi zoezi la Uboreshaji wa daftari la Kudumu la Wapiga kura ifikapo tarehe 01 Machi 2025 litakalodumu kwa muda wa siku 7, hadi tarehe 07 Machi 20225.
Yamebainisha hayo leo tarehe 22 Februari 2025, na Makamu Mwenyekiti wa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe Jaji Rufaa ( Msaafu) Mbarouk Salimu Mbarouk wakati wa uzinduzi wa Mafunzo kwa Watendaji ngazi ya Jimbo kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika ukumbi wa mikutano wa YMCA, Wilayani Pangani.
Akiongea mala baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo makamu mwenyekiti wa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Rufaa (mstaafu )Mbarouk S Mbarouk amewataka maafisa hao kuwahudumia watu kwa upole ili shughuli hii ifanyike kwa weledi kwa manufaa makubwa ya Taifa letu.
" Shughuli ya Uboreshaji wa daftari la Kudumu la Wapiga kura ni la Kitaifa hivyo ni shughuli muhimu sana. Alifafanua".
Kauli mbiu, " Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora".
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa